1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti mpya yaonesha machafuko yauwa watu elfu 15 DRC

24 Mei 2022

Ripoti mpya inaonesha kwamba watu zaidi ya 15000 wamepoteza maisha katika mauaji ya kila mara yakiyofanyika mashariki ya Congo tangu miaka 15 hususan katika mikoa ya Ituri, Kivu kaskazini na hata pia Kivu Kusini.

Demokratische Republik Kongo | Unruhen in Beni
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Ripoti hii iliyochapishwa na kutetewa na wabunge wawili kutoka Kivu Kaskazini wanaounga mkono rais Félix Tshisekedi inaonesha kwamba ni maeneo ya Beni katika Kivu Kaskazini, Irumu na Mambasa katika mkoa wa Ituri ambayo yamekuwa wahanga zaidi wa mauaji haya tangu miaka kumi na tano iliyopita. Maeneo haya yanakabiliwa na tishio kutoka kwa waasi wa Uganda ADF walio jihifadhi nchini Congo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa kutoka elfu mbili nane hadi elfu mbili kumi na mbili mauaji hayakuwa makali. Kisha kati ya elfu mbili kumi na tatu na elfu mbili kumi na nane takwimu zililipuka hadi kufikia elfu nane watu waliokufa, na kwamba maeneo fulani yalishambuliwa na ADF mara kadhaa kwa mwaka.

Mbusa Mbeze ni miongoni mwa wabunge wanaotetea ripoti hiyo amesema "Katika elfu mbili na ishirini kwa mfano, mashambulizi mia mnane tisini na nane (898) yalirekodiwa na kusababisha waathiriwa elfu mbili mia sita tisini na tano (2695), na mnamo 2021, mashambulio 1019 yalirekodiwa na kusababisha wahasiriwa elfu ine mia nne ishirini na mnane (4428)”.

Watu elfu tano wamekufa tangu kuanza kwa utawala wa kijeshi Kivu Kaskazini.

Wapiganaji waasi wa DRCPicha: Lionel Healing/AFP/Getty Images

Ripoti hyo inataja vifo vya karibu watu elfu tano tangu kuanzishwa kwa utawala wa kijeshi huko Kivu Kaskazini na Ituri mwaka mmoja uliopita. Pia, inajumuisha majina na picha za wahasiriwa wote, na wabunge hao wanaamini kwamba inaweza kutumika kama ushahidi mahakamani ikiwa ni lazima. Mbunge Tembo Siyotama ni miongoni mwa waanzilishi wa ripoti hiyo:

"Leo katika eneo linalodhibitiwa na wanaodhaniwa kuwa ADF, ikiwa hao watu elfu kumi na tano waliokufa wanawaze kutafutwa, tunaweza kuwapata katika ripoti hii, na tunaweza kwenda na kutambua anwani zao kwa sababu siku moja haki lazima itendeke. Kadiri muda unavyopita, ndivyo tunavyosahau zaidi”.

Pamoja na kutambuwa hali ya ukosefu wa usalama, utawala umetambua changamoto za kiusalama na kukumbusha juhudi za rais Félix Tshisekedi kutafuta amani mashariki ya Congo, lakini pia ukijiswalli kuhusu idadi hiyo iliyotangazwa. James Karani ni miongoni mwa wanachama wakuu wa chama tawala cha UDPS mjini Bukavu.

Soma zaidi:Tshisekedi akamilisha ziara yake Burundi 

Wakati huo huo, mapambano yameripotiwa jana jumatatu kati ya jeshi la Congo FARDC na waasi wa M23 katika eneo la Ruthshuru, si mbali na nchi ya Rwanda. Katika ùkoa wa Kivu kusini pia mapambano makali yameripotiwa siku hiyohiyo kule Bigaragara katika Maeneo ya Minembwe. Duru mbalimbali zimeshuhudia kwamba watu ine wamepoteza maisha.

DW, Bukavu

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW