UhalifuKimataifa
Ripoti: Wanaharakati wa mazingira 142 waliuawa 2024
17 Septemba 2025
Matangazo
Hayo ikiwa ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika lisilo la kiserikali la Global Witness. Ripoti hiyo inasema wengi ya waliolengwa walikuwa wakipigania haki za watu wa jamii za asili au wakulima wadogo.
Wengine ni pamoja na wale waliokuwa wanapambana dhidi ya uchimbaji haramu wa madini, biashara ya magogo, ujangili na miradi ya nishati.
Kulingana na ripoti, kwa mara nyingine Colombia imeongoza kwa idadi kubwa ya vifo 48 vya wanaharakati wa mazingira ikifuatiwa na Guatemala, Mexico na Brazil.
Watafiti wamesema mauaji mengi yalifanywa na makundi ya wahalifu na katika baadhi ya matukio vyombo vya usalama wa taifa vilihusika.