1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Shirika la kupigania nhaki za binadamu duniani, Human Rights Watch, juu ya mateso wanayofanyiwa wafungwa wa Iraq na majeshi ya Kimarekani.

23 Julai 2006

Katika ripoti yake iliotolewa leo, Shirika la kupigania haki za binadamu duniani, Human Rights Watch, limesema kwamba makamanda wa jeshi la Marekani waliutilia moyo mtindo wa kuwatukana kwa matusi wafungwa huko Iraq pale wanapowahoji, hata baada ya kufichuliwa kashfa katika Gereza la Abu Ghraib hapo mwaka 2004. Ripoti hiyo ilisema baina ya mwaka 2003 na 2005, wafungwa walikuwa wakitendewa vibaya kila wakati, wakinyimwa nafasi ya kulala na kuwekwa katika joto kali kama sehemu ya mwenendo wa kuwahoji. Shirika hilo limesema limeyajua hayo baada ya kuwahoji maafisa wa kijeshi na kusoma taarifa za viapo za watu walioathirika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW