1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Umoja wa mataifa kuhusu njaa ulimwenguni

Oumilkher Hamidou15 Oktoba 2009

Idadi ya wasiokula vya kutosha na wanaokufa kwa njaa imeongezeka sana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita

Mkurugenzi mkuu wa shirika la WFP bibi Josette Sheeran na mwenyekiti wa shirika la FAO Jacques DioufPicha: AP


Zaidi ya watu bilioni moja wanasumbuliwa na njaa ulimwenguni mnamo mwaka huu wa 2009,hali ya kusikitisha iliyosababishwa na mchanganyiko wa uhaba wa chakula na mgogoro wa kiuchumi.

Mchanganyiko wa uhaba wa chakula na mgogoro wa kiuchumi umepelekea kuongezeka vibaya sana idadi ya wenye njaa ulimwenguni-zaidi ya watu bilioni moja- hawali vya kutosha"imetajwa katika ripoti ya mwaka 2009 ya shirika la umoja wa mataifa la Chakula na Kilimo-FAO,iliyoandaliwa kwa ushirikiano pamoja na Mpango wa chakula ulimwenguni-WFP.

Idadi ya wahanga wa ukosefu wa chakula bora imeongezeka kwa watu milioni mia moja ikilinganishwa na mwaka jana na kufikia kiwango cha juu kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu miaka 40 iliyopita-imetajwa katika ripoti ya ya mashirika hayo mawili ya umoja wac mataifa FAO na WFP.

"Si jambo linaloweza kukubalika kuona idadi kubwa kama hii ya watu wakisumbuliwa na njaa" amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la Chakula na kilimo FAO, Jacques Diouf alipokua akichambua ripoti hiyo.

"Tuna njia za kiuchumi na kiufundi za kusitisha njaa,kinachokosekana ni dhamiri za dhati za kisiasa za kupiga vita njaa moja kwa moja"Amesisitiza Jacques Diouf.

Mratibu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki ya chakula Olivier Schutter anasema anaamini mapambano dhidi ya njaa yanaweza kufanikiwa ikiwa juhudi zitalengwa zaidi katika kuwekeza katika sekta za kilimo badala ya kuhimiza viwango vya mazao ya mashambani vizidishwe.

Mtoto mdogo anaramba sufuria-hajashibaPicha: dpa

Wataalam wanakubaliana kuna chakula cha kutosha katika ardhi yetu kuweza kumlisha vya kutosha kila mkaazi wa dunia hii.

Mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya mazingira Achim Steiner anasema dunia ina chakula cha kutosha kupita hata mahitaji yaliyoko.Wakaazi wote wa dunia wanaweza kujipatia chakula cha kutosha bila ya watu kuwa na haja ya kupanua hata kilomita moja ya mraba ya ardhi yetu.Achin Steiner anaendelea kusema:

"Watu hawazingatii kwamba,katika wakati ambapo kuna mgogoro jumla wa chakula na uhaba wa chakula,asili mia kati ya 30 hadi 40 ya mazao ya chakula yanamwagwa.Yanaangamia kutokana na utaratibu wa uzalishaji na pia uuzaji wa bidhaa.Badala ya kutafakari,ardhi ziada tutaipata wapi,au tutabidi kukimbilia mwezini,ili kuweza kupata chakula cha kutosha,tunabidi kwanza tuangalie huku huku duniani tuliko."

Wakati huo huo muasisi wa kampuni ya mitambo ya Computor- Microsoft, mfadhili wa kimarekani Bill Gates ametangaza kitita cha dala milioni 120 kusaidia kuimarisha usalama wa chakula barani Afrika na nchini India.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir(Reuters/AFP)

Mhariri:Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW