1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Umoja wa mataifa: -Wakaazi duniani kuongezeka 2300, hadi bilioni 9.

10 Desemba 2003
Baada ya kupanda na kushuka kwa idadi ya watu duniani, sasa makadirio mapya ya Umoja wa mataifa ni kwamba idadi hiyo itaongezeka mno na kufikia bilioni 9 ifikapo mwaka 2300. Ama mkurugenzi wa idara inayohusika na wakazi duniani ya umoja wa mataifa Joseph Chamie anasema" hiki ni kiroja",kwani hakuna ajuwae hali itakuaje miaka inayokuja. Lakini wanachojaribu ni kutoa sura ya kile kinatakachoweza kutokea Makadiro hayo yanatokana na dhana ya matarajio ya kuongezeka kwa kiwango cha kuishi kikiambatana wakati huo huo na fikra ya kwamba muda mrefu ujao, wanawake watakua na wastani wa watoto wawili tu.
Ikiwa kiwango cha uzazi kitabakia kama kilivyo sasa, basi idadi ya watu duniani itafikia trilioni 134 miaka 300 ijayo. Mkurugenzi Chamie anasema hili linashangaza kwani idadi ya wakazi itapindukia hata maeneo yaliofurika zaidi binadamu duniani hii leo, kama vile Hong Kong yenye wastani wa zaidi ya watu 100 kwa kila mita moja ya mraba ya ardhi.Lakini hata kama wanawake watakua na idadi zaidi kidogo ya watoto watakaozidi wawili, basi kwa wastani idadi ya watu duniani inaweza pia kuongezeka sana na kama uzazi utapungua chini ya watoto wawili kwa kila mwanamke, basi ifikapo 2300 watakua wanaishi watu 2.35 bilioni duniani.
Ama idadi ya watu haitaongezeka kwa kiwango sawa katika sehemu zote za dunia. Wakati barani ulaya itapungua kutoka asili mia 14 hadi asili mia 7, barani afrika itaongezeka mara dufu kutoka asili mia 13 hadi asili mia 24 fikapo 2300. India, China na Marekani zitaendelea kuwa nchi zenye idadi ya watu wengi zaidi ulimwenguni.
Ongezeko kubwa kabisa la idadi ya watu duniani litakua katika nchi masikini ambazo hazitakua na uwezo wa kumudu ongezeko hilo na hasa huko kusini mwa Asia , Mashariki ya kati na barani Afrika.
Bw Chamie anaeleza kwamba Misri kwa mfano tayari inapaswa kuagiza zaidi ya theluthi moja ya chakula cha msingi kutoka n´gambo, lakini pamoja na hayo italazimika kuwa na watu milioni 10 zaidi.
Kwa mujibu wa afisa huyo wa umoja wa mataifa, tatizo si uhaba wa chakula duniani. Akiongeza kuwa"Kuna chakula kingi kwa watu kati ya bilioni 6 na bilioni 9 lakini tatizo kwa jumla ni usambazaji, pato la kutosha na uwezekano wa kukipata chakula hicho."
Umri wa wastani wa kuishi 2300 -kwa mujibu wa ripoti hiyo- utakua karibu miaka 50. Hivi sasa ni miaka 26 na karibu asili mia 40 ya wakaazi watakua wazee wa zaidi ya umri wa miaka 60. Athari za kuwa na idadi kubwa ya watu wenye umri wa juu kwa mfano katika nchi zilizoendelea , ni katika masoko ya ajira ambapo watalazimika kufanya kazi kwa masaa mengi zaidi, marupurupu yakiwa madogo zaidi, huku wakilipa kodi kubwa zaidi kuwagharimia watoto na watu wazee. Kwa nchi zinazoendelea na zile masikini, wiwapo wanawake wataendelea kutaka kuwa na watoto zaidi, hali hiyo itapunguza kiwango cha ukuaji wa uchumi kuliko ilivyo hivi sasa .
Kwa wanawake katika nchi zilizoendelea sababu kubwa ya kuweko kwa idadi ndogo ya watoto ni kwamba wana matatizo kuoanisha ajira na huduma kwa familia na kutokana na hayo idadi ya wakaazi inaelekea kupungua na wasi wasi utazidi katika sekta ya wafanyakazi kuelekea idadi ya wanaostaafu na watoto .
Ripoti inaashiria pia kwamba ukimwi utaendelea kuwa na athari kubwa hasa kwa eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara . Makadirio ya idadi ya watu duniani 2050 yamepunguzwa kwa milioni 2000 kwa sababu ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo. Lakini pakitarajiwa mabadiliko katika tabia za binaadamu, inatarajiwa hali itakua bora zaidi kuliko ilivyo hii leo.
Ripoti hiyo ya umoja wa mataifa ni ya kwanza kuhusiana na mtazamo wa idadi ya wakaazi kuzingatia kipindi cha miaka 300 ijayo ikitoa mtazamo wa nchi fulani na sio tu wa maeneo ya kimkoa.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW