Ripoti ya UN yawatuhumu maafisa wa Sudan Kusini kwa ukiukaji
4 Aprili 2023Katika ripoti iliyotolewa jana Jumatatu na tume ya haki za binadamu ya Sudan Kusini, gavana wa jimbo la kusini la Unity, Joseph Monytuil ametajwa kuwa na dhamana kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu pamoja na maafisa wa vyeo vya juu serikalini na jeshini.
Soma pia:Umoja wa Mataifa wataka kusimamishwa mapigano Sudan Kusini
Ripoti hiyo inasema Luteni Jenerali Thoi Chany Reat wa jeshi la Sudan Kusini ni miongoni mwa watu wanaotakiwa wachunguzwe kwa mauaji ya kiholela yaliyoendeshwa na serikali katika kaunti ya Mayom mnamo Agosti 2022.
Ripoti ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa inasema Sudan Kusini sharti ikabiliane na tabia ya watu kufanya uhalifu bila hofu ya kuwajibishwa kisheria ili kudhibiti machafuko ya mara kwa mara na ukiukaji wa haki za binadamu.