Ripoti ya Usalama Munich
20 Februari 2017Ripoti hiyo pia imekusanya habari juu ya vitisho vya wapiganaji wa jihadi, upoteshaji wa habari na pia utumiaji wa habari kama silaha pamoja na hali ya usalama katika eneo la bahari ya Pasifiki na mashariki ya kati.
Wolfgang Ischinger, mkuu wa mkutano wa kimatifa wa usalama duniani,ameandika kuwa usalama duniani kwa sasa ni tete ukilinganishwa na wakati wowote ule tangu kumaliza kwa vita vikuu vya pili vya dunia, na vile vile tokea kumalizika kwa ukoloni wa nchi za magharibi na kutawala kwa siasa za kiliberali katika mfumo wa amani duniani. Sababu za kusema hayo ni pamoja na odhaifu uliopo katika umoja wa ulaya,usambazaji wa habari na pia uteuliwa wa Trump kuwa rais mpya wa Marekani.
Juu ya hayo pia kuna mjadala wa habari bandia na habari potofu, ambazo sasa zimekuwa pia changamoto katika uandikaji na uenezaji wa habari.
Changamoto zinazoikabili dunia katika maswala ya usalama
Hofu katika jamii zilizowazii hazianzi kutoka ndani peke yake, bali pia zinaanza na habari zisizoridhisha ambazo husambaa ndani ya jamii yenyewe.
Lakini changamoto kubwa katika usalama wa kimataifa, lipo katika makundi ya jihadi, yenye wafuasi pia katika nchi za magharibi. Wafanya mashambulizi Ulaya, wengine hutumia jina la jihadi kufanya mashambulizi hayo. Nchi za ulaya pia hutafautiana katika jinsi ya wanavyokabiliana na vikundi vya ugaidi. Kwa mfano Ufaransa wao, walitangaza kuwa nchi yao iko katika hali ya dharura, na huku Ujarumani hutumia njia ya kuvamia makaazi ya washambulizi na sehemu nyengine.
Kurasa 90 za repoti ya mkutano wa Munich wa usalama duniani, inatupa mtazamo, wa matatizo ya kisiasa ya dunia. Mwandishi wa ripoti hiyo ameandika undani wa mikakati ya muelekeo utakaoweza kuumaliza mfumo wa dunia uliowekwa baada ya vita vikuu vya pili vya dunia na ambao unaweza kuathirika kwa kuzuka siasa kali za kizalendo katika bara la Ulaya.
Kwa sasa kunaoneka kuna udhaifu katika ushirikiano baina ya nchi kadhaa pamoja na kuweko kwa migogoro baina ya nchi mbali mbali.
Muandishi: Najma Said
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman