1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rishi Sunak kukutana na Rais Emmanuel Macron mjini Paris leo

10 Machi 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anatarajiwa kukutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo Ijumaa.

Cop27 -  Rishi Sunak und Emmanuel Macron
Picha: Steve Reigate/Daily Express/empics/picture alliance

Viongozi hao wawili watakubaliana juu ya ushirikiano wa karibu wa ulinzi na usalama pamoja na usaidizi zaidi kwa Ukraine na katika kanda ya Indo-Pasifiki.

Sunak anakutana na Macron mjini Paris, akiwa ameambatana na mawaziri kadhaa, wakati mataifa hayo mawili yakijaribu kurekebisha uhusiano wake ambao ulidhoofika mara baada ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kwa kiasi fulani umeonekana kuimarisha mahusino baina ya nchi hizo mbili. Kuelekea mkutano wa leo, ofisi ya waziri mkuu Sunak, ilisema kwamba Uingereza na Ufaransa  zitaratibu utoaji wa silaha kwa Ukraine na mafunzo ya jeshi la wanamaji wa Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW