1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Rishi Sunak na Emmanuel Macron wakutana Paris

10 Machi 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amekutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Paris katika juhudi za kuimarisha mahusiano

Paris | Sunak bei Macron
Picha: Emmanuel Dunand/AFP

Mkutano huo wa kilele pia unakusudia kuondoa mivutano ya miaka kadhaa baada ya Brexit na kufikia makubaliano mapya kuhusu ujia wa bahari unaotumiwa na wahamiaji mpakani mwa nchi hizo mbili.

Kuelekea mkutano wao wa kilele, ambapo walitarajiwa kuzungumzia pia usaidizi wao kwa Ukraine na usalama wa kanda ya Asia-Pasifiki, Sunak alisifu uhusiano baina ya nchi hizo jirani akisema ni muhimu.Rishi Sunak na Emmanuel Macron kujadili uhamiaji na Ukraine

Baada ya kusafiri kwa treni kutoka London, Sunak alipokelewa na mwenyeji wake Emmanuel Macron kwenye ikulu yake mjini Paris.

Huo ni mkutano wa kwanza wa kilele kati ya Ufaransa na Uingereza ndani ya miaka mitano.

Mkutano huo umejiri takriban miezi sita tangu Rishi Sunak kuchukua madaraka mwezi Oktoba mwaka uliopita, baada ya watangulizi wake Liz Truss na Boris Johnson waliolazimika kujiuzulu kufuatia misukosuko ya kisiasa.

Mkutano kati ya Rishi SUnak na mwenyeji wake Emmanuel Macron ndio wa kwanza wa kilele ndani ya miaka mitano.Picha: Le Pictorium/Imago

Chuki ya Macron kwa Boris Johnson alipokuwa waziri mkuu haikufichika. Naye Truss, wakati wa kampeni zake kuwa waziri mkuu aliwahi kusema hakujua kama Macron alikuwa rafiki au adui.

Uingereza yatangaza sheria inayokusudiwa kuzuwia maelfu ya wahamiaji wanaowasili nchini humo

Lakini kwa sasa, tawala hizo zina nafasi ya kurekebisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu ya silaha za nyuklia Magharibi mwa Ulaya.

Mnamo Alhamisi, Sunak alisema kupitia taarifa kwamba "Historia yao ndefu, ukaribu wao, na mtizamo wao wa pamoja kuhusu masuala ya kimataifa, vyote vinamaanisha kuwa ushirikiano imara kati ya Uingereza na Ufaransa ni ya thamani na umuhimu mkubwa.

Uingereza pia imeimarisha uhusiano na Umoja wa Ulaya

Mkutano huo umejiri wakati uhusiano kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya pia umeimarika kufuatia kile kiitwacho 'Makubaliano ya Windsor' yanayolenga kusuluhisha matatizo yaliyoibuka na Ireland ya Kaskazini baada ya Brexit. Uingereza na EU zafikia mkataba wa baada ya Brexit

Sunak alithibitisha kuwa nchi yake pia itakuwa mwenyeji wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya, mpango wa Macron ulioanzishwa baada ya Urusi kuivamia Ukraine. Baadaye mwezi huu, Mfalme Charles III wa Uingereza pia atazuru Ufaransa.

​​​​Emmanuel Macron na Rishi SUnak wanatarajiwa kujadili pia jinsi ya kuimarisha uzuiaji wa uhamiaji usiokubalika katika ujia wa Uingereza baharini.Picha: SAMEER AL-DOUMY/AFP/Getty Images

Mnamo Novemba, Uingereza na Ufaransa zilisaini makubaliano yenye thatamani ya euro milioni 72 kuimarisha juhudi za kuzuia wahamiaji wasiokuwa na vibali wanaofunga safari hatari baharini katika ujia wa Uingereza.

Udhibiti wa uhamiaji kupitia ujia wa Uingereza baharini ni moja ya ajenda ya mkutano wao

Sunak aliwaambia waandishi habari kwamba kipaumbele chake cha kwanza ni kuimarisha ushirikiano utakaozuia uhamiaji huo.

Uingereza imekuwa ikiilipa Ufaransa kushika doria katika ujia huo wa mpakani. Mshauri mmoja wa Macron amesema mazungumzo ya viongozi hao yatalenga pia kuimarisha nyenzo za kusimamia ujia huo kila mwaka.

Kulingana na ofisi ya Sunak, viongozi hao pia watakubaliana kuhusu taratibu zinazohitajika za kuendelea kuipa Ukraine silaha na kuwapa wanajeshi wake mafunzo.

Vyanzo: AFPE, RTRE

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW