1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rivers United ya Nigeria yaishinda 3-0 Academica Lobito

27 Novemba 2023

Klabu ya Rivers United ya Nigeria ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Academica Lobito ya Angola katika mechi ya kusisimua ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Africa CAF iliyochezwa jana Jumapili.

Fußball CAF Confederation Cup | Young Africans - USM Alger
Picha: Sports Inc/empics/picture alliance

Ndani ya dakika tatu tu Klabu hiyo ilifanikiwa kupata bao la kwanza lililotiwa wavuni  na Samuel Antwi, huku Paul Odeh na Shadrack Asiegbu wakifunga bao la pili na tatu mtawalia katika kipindi cha pili.

Rivers inaongoza kundi C kwa tofauti ya mabao, mbele ya Club Africain ya Tunisia, iliyoifunga Dreams ya Ghana mabao 2-0 mjini Rades.

Ushindi huo umewapa matumaini Rivers United kuwa klabu ya kwanza kutoka Nigeria kuwahi kushinda Kombe la Shirikisho barani Africa.

Mara ya mwisho kwa klabu ya Nigeria kufika fainali ya michuano hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2005 wakati Dolphins ilipofungwa na FAR Rabat ya Morocco.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW