1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH : OPEC yamalizika mkutano kwa tafauti ya kisiasa

19 Novemba 2007

Mkutano wa Jumuiya ya OPEC ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani umemalizika hapo jana kwa tafauti kubwa za kisiasa iwapo ama la kuchukuwa hatua juu ya sarafu dhaifu ya dola wakati wakuu wa nchi hizo wakiahidi kuendelea kuwapatia mafuta ya kutosha watumiaji wa mataifa ya magharibi.

Kuanguka kwa thamani ya sarafu ya dola kwenye masoko ya dunia kumesaidia kupandisha bei ya mafuta kufikia dola 98 kwa pipa ambayo haikuwahi kufikiwa kabla hapo tarehe saba Novemba na kusababisha mataifa ya magharibi kutowa wito kwa OPEC kutuliza bei za mafuta hatua ambayo pia imedhoofisha nguvu ya ununuzi ya nchi wanachama wa OPEC.

Taarifa ya mwisho ya mkutano huo wa viongozi wa nchi wanachama wa OPEC katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh haikutaja kitu juu ya hatima ya dola ukiwa ni ushindi kwa washirika wa Marekani wenye msimamo wa wastani wakiongozwa na Saudi Arabia.