RIYADH: Umoja wa Ulaya na nchi za Ghuba zajadili biashara huru
8 Mei 2007Matangazo
Maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya wakiongozwa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier hii leo wanakutana mjini Riyadh,Saudi Arabia kwa mazungumzo pamoja na nchi sita za Kiarabu zilizo wanachama wa AGCC.Mada kuu inahusika na mkataba wa biashara huru.Viongozi hao wanatumaini kuwa makubaliano ya biashara yataweza kutatiwa saini kipindi cha hivi sasa ambapo Ujerumani imeshika wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka kila miezi sita.Kwa mujibu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya,mkataba huo utaweza kuongeza maradufu biashara kati ya Ulaya na nchi za Ghuba ya Kiarabu.