1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robert Habeck kuchaguliwa kukiongoza chama cha Kijani

17 Novemba 2024

Chama cha Kijani cha walinzi wa mazingira nchini Ujerumani kitamteua mgombea wa ukansela atayekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao

Hatua hiyo itafikiwa mwishoni mwa kongamano la siku tatu la chama hicho linalomalizika hii leo Jumapili. Waziri wa Uchumi Robert Habeck ana nafasi kubwa kubwa zaidi ya kuchaguliwa kukiongoza chama cha kijani kuliko mpinzani wake mkubwa Waziri wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock, aliyegombea ukansela kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2021.

Soma Pia: Mkwamo wa bajeti watishia kuivunja serikali ya Ujerumani

Baerbock alisema mnamo mwezi Septemba kwamba safari hii hatagombea. Robert Habeck, ambaye pia ni makamu wa kansela katika serikali ya Kansela Olaf Scholz wiki hii alithibitisha mipango yake ya kugombea nafasi hiyo ya juu.