Robert Mueller: aliyeiongoza FBI Marekani afariki dunia
22 Machi 2026
Kifo chake kimesherehekewa hadharani na rais Trump.
Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti vikinukuu taarifa ya familia ya Mueller kwamba mkurugenzi huyo wa zamani aliaga dunia Ijumaa jioni bila ya kutoa sehemu alipofia wala sababu ya kifo chake.
Baada ya tangazo hilo, rais Donald Trump aliandika katika mtandao wake wa Truth Social kwamba na hapa namnukuu " Robert Mueller amefariki, vizuri, nafurahi amekufa, na kwamba hawezi kuwaumiza tena watu wasiokuwa na hatia!" mwisho wa nukuu.
Licha ya kauli yake hiyo marais wengine wa zamani walijibu taarifa ya kifo cha Muller kwa kumtaja vizuri.
Barack Obama alimsifia Mueller akisema ni mfanyakazi aliyeheshimika kutokana na kazi yake huku George W. Bush, akisema amesikitishwa na kifo cha mueller aliyejitolea kuitumikia Marekani kwa nguvu zake zote.