Roberta Metsola achaguliwa tena spika wa bunge la Ulaya
16 Julai 2024Matangazo
Roberta Metsola amechaguliwa tena kwa muhula wa pili kama spika wa Bunge la Umoja wa Ulaya, katika mkutano wa kwanza wa wabunge huko Strasbourg, mashariki mwa Ufaransa.
Metsola kutoka Malta aliyepata kura 562, atakuwa spika kwa miaka mingine miwili na nusu, baada ya chama chake cha mrengo wa kulia cha EPP kujishindia viti 188 katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya mwezi uliopita.
Siku ya Alhamisi wabunge hao wanatarajia pia kumchagua Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya na Ursula von der Leyen huenda akajishindia muhula wa pili, licha ya matokeo ya kura hiyo kutotabirika.