1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rodri ashinda Ballon d'Or, Madrid wasusia

29 Oktoba 2024

Kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Rodri ameshinda tuzo ya mchezaji bora duniani ya Ballon d'Or. Rodri alishinda taji la Ligi ya Premier ya England na la Euro 2024.

Paris | Rodri ashinda Ballon d'Or
Kiungo wa Manchester City na Uhispania Rodri ashinda Ballon d'Or 2024Picha: Michel Euler/AP Photo/picture alliance

Uamuzi wa kumtuza kiungo huyo mkabaji ulipokelewa kwa mshangao kwa vile mshindi wa taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya Vinicius Junior wa Real Madrid alionekana kupigiwa upatu na wengi.

Saa chache kabla ya hafla hiyo ya jana usiku mjini Paris, klabu hiyo ya Uhispania ilitangaza kuwa ujumbe wake hautahudhuria sherehe hiyo kwa sababu ya kile ilichokichukulia kuwa ni kutotendewa haki Vinicius.

Soma pia: Lionel Messi aweka rekodi kwa kushinda tuzo ya nane ya Ballon d'Or

Rodri, mwenye umri wa miaka 28 alichangia pakubwa wakati City iliizuia Arsenal kushinda Ligi kuu ya England msimu uliopita na alitajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Euro 2024 wakati Uhispania iliibuka mshindi nchini Ujerumani.

Staa wa Barcelona na Uhispania Aitana Bonmati alishinda tuzo yake ya pili mfululizo ya Ballon d'Or ya wanawake. Aliiongoza klabu yake kuweka historia ya kushinda mataji manne katika msimu mmoja na pia taji la Nations League na timu ya taifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW