1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Kandanda

Rodri atajiunga na Barcelona?

10 Agosti 2026

Nahodha wa Uhispania na Manchester City Rodri anatarajiwa kuihama klabu hiyo ya England na kujiunga na Barcelona ambao ndio mabingwa wa Uhispania.

Nahodha wa Uhispania Rodri
Nahodha wa Uhispania RodriPicha: Andrew Milligan/empics/picture alliance

Kwa sasa ripoti zinaarifu kuwa vilabu hivyo viwili viko katika mazungumzo ingawa kocha wa City Maresca amesema anamtarajia Rodri arudi kujiunga na wachezaji wenzake kwa mazoezi ya kabla msimu kuanza.

Awali Rodri alikuwa anawindwa na Real Madrid pia ila kama ilivyotarajiwa na wengi hangeweza kujiunga na Madrid ukizingatia aliwahi kuichezea Atletico Madrid na kwa kuzingatia pia uhasama uliopo kati ya vilabu hivyo viwili vya Madrid.

Rodri alitawazwa kama mchezaji bora wa Kombe la Dunia lililokwisha huko Marekani mwezi uliopita wa Julai.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW