ROMA: Euro milioni 360 kutolewa kuisadia Afghanistan
4 Julai 2007Wadhamini wa kimataifa wameahidi kutoka euro milioni 360 kuisaidia Afghanistan kuanzisha mfumo mpya wa sheria.
Kwenye mkutano uliofanyika mjini Roma Italia, rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, alisisitiza kuwa swala la haki litaendelea kubakia kuwa ndoto ikiwa ugaidi utaendelea kufanyika karibu kila siku nchini humo. Hata hivyo alidokeza kuwa juhudi za Afghanistan kuelekea demokrais zinahitaji mda.
Wakati huo huo, katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi, NATO, Jaap de Hoop Scheffer, ameahidi kuchunguza vifo vya raia nchini Afghanistan.
Hata hivyo alisema mambo yanayofanywa na jumuiya NATO nchini Afghanistan hayawezi kulinganishwa na maovu yanayofanywa na wanamgambo wa kundi la Taliban ambao huwakata watu vichwa, kuchoma shule na kuwaua wanawake na watoto.