ROMA: Licha ya mavuno bora katika baadhi ya nchi za kiafrika,...
9 Desemba 2003Matangazo
bado waafrika kwa mamillioni wanateseka kwa njaa. Nchi kama 23 zitaraji shida ya chakula siku mbele, - lilitangaza shirika la Chakula na Kilimo FAO la Umoja wa Mataifa mjini Roma. Katika pembe ya Afrika, watu millioni zaidi ya moja wanahitaji msaada wa chakula Eritrea, na laki 93 nchini Somalia. Licha ya kuboreka hali ya hewa kwa mavunao yajayo, wananchi millioni tano na nusu wataendelea kutegemea msaada wa kigeni nchini Zimbabwe. Na hata Angola, licha ya kuboreka mavuno mwaka jana, watu zaidi ya millioni moja watahitaji misaada.