ROMA: Prodi apata uungwaji mkono
23 Februari 2007Viongozi wa serikali ya mseto ya mrengo wa kati na kushoto nchini Italia wamekubaliana kumuunga mkono bwana Romano Prodi aendelee kubakia madarakani kama waziri mkuu wa nchi hiyo.
Makubaliano hayo yanafuatia mkutano uliofanywa jana usiku huku Prodi akijaribu kutafuta uungwaji mkono katika juhudi za kuunda serikali mpya.
Romano Prodi alijiuzulu juzi Jumatano baada ya serikali yake ya mseto kushindwa kwenye kura iliyopigwa bungeni. Mswada uliopigiwa kura ulihusu mpango wa kurefusha muda wa wanajeshi 2,000 wa Italia walio nchini Afghanistan na upanuzi wa kambi ya jeshi la Marekani katika mji wa kaskazini wa Vicenza.
Rais Giorgio Napolitano wa Italia, amekuwa akifanya mazungumzo ya dharura kujaribu kuutanzua mzozo huo wa kisiasa. Atanatakiwa kuamua ikiwa waziri mkuu Prodi au kiongozi mwengine ataunda serikali mpya ya mseto au aitishe uchaguzi mpya nchini Italia.