ROMA: Watu kumi wahukumiwa kifungo cha maisha nchini Italia kwa mauaji ya Kinazi.
14 Januari 2007Matangazo
Mahakama ya Italia imewapata na hatia watu kumi waliokuwa maafisa na askari wa utawala wa Hitler.
Washukiwa hao wamepatikana na hatia ya makosa waliyotenda zaidi ya miaka sitini iliyopita katika Vita vya Pili vya Dunia wakati Manazi wa kijerumani walipowaua raia kaskazini mwa Italia.
Washukiwa hao, ambao wana umri kuanzia miaka themanini, hawakuwepo mahakamani wakati walipohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Mwaka elfu moja mia tisa na arobaini na nne maafisa wa kijasusi wa utawala wa Hitler waliwaua raia kiasi mia saba katika kijiji cha Marzabotto karibu na Bologna.
Raia hao waliouawa wengi wao walikuwa wanawake, watoto na wazee.
Hilo ndilo lililokuwa tukio baya zaidi la mauaji nchini Italia wakati wa vita.
Mwaka elfu mbili na mbili Rais wa Ujerumani wa wakati huo Johannes Rau alisikitishwa na hali ilivyokuwa alipozuru Marzabotto.