ROMA:Hali ya ukame yaifanya Italia kutangaza hali ya dharura
4 Mei 2007Matangazo
Italia imetangaza hali ya dharura katika maeneo ya kaskazini na kati ya nchi hiyo kutokana na hofu ya ukame kufuatia hali mbaya ya hewa.
Waziri wa Mazingira wa Italia Alfonso Pecoraio Scanio, amesema kuwa hali hiyo imetangazwa kama hatua za tahadhari.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya nchi jirani na Italia, Ufaransa, kutangaza mgawo wa maji katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo kwa hofu pia ya ukame.