ROME: Berlusconi akubali kuunda serikali mpya
23 Aprili 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Uitalia,Silvio Berlusconi aliezongwa na matatizo,amekubali kuunda serikali mpya ili kujiepusha na mzozo wa kisiasa na vile vile kuzuia kuitisha uchaguzi mpya kabla ya wakati wake.Rais Carlo Azeglio Ciampi wa Uitalia amemtaka Berlusconi aunde serikali mpya siku mbili baada ya Berlusconi kulazimishwa kujiuzulu na washirika wake kwenye serikali ya mseto.Berlusconi amesema ameafikiana na washirika wake kuunda serikali mpya ya muungano na wiki ijayo anatazamia kulitangaza bungeni,baraza jipya la mawaziri wake kupigiwa kura ya imani.