1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Italia yaitaka Marekani kuheshimu uhuru wa kujitawala wa nchi hiyo.

2 Julai 2005

Waziri mkuu wa Italia Bwana Silvio Berlusconi ameitaka Marekani kuheshimu uhuru wa nchi hiyo. Hii inafuatia ripoti kuwa wafanyakazi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA wamemteka nyara kiongozi wa dini ya Kiislamu mjini Milan miaka miwili iliyopita.

Berlusconi ametoa taarifa hiyo baada ya kumuita balozi wa Marekani kutaka maelezo zaidi juu ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa ripoti, CIA wamevunja sheria za Italia kwa kumkamata kiongozi huyo wa dini na kumpeleka Misr, ambako inaaminika kuwa aliteswa.

Wiki iliyopita, jaji mmoja mjini Milan alitoa hati ya kukamatwa wafanyakazi 13 wa CIA wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo la utekaji nyara.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW