Rome. Juve yashushwa Serie B.
15 Julai 2006Matangazo
Mahakama yenye jukumu la kutoa hukumu katika kashfa ya kupanga matokeo ya mchezo wa kandanda nchini Italia imeamuru vigogo vya soka nchini humo, Juventus Turin , Fiorentina na Lazio kushushwa daraja la pili Serie B pamoja na adhabu ya kupoteza pointi.
Shirikisho la kandanda nchini Italia limesema mahakama hiyo pia imeamuru kuwa AC Milan itabaki katika daraja la kwanza Serie A lakini jumla ya ponti zake ilizopata katika msimu uliopita 44 , zitapunguzwa uamuzi ambao utasababisha timu hiyo kutokuwamo katika kinyang’anyiro cha kombe la mabingwa wa Ulaya , Champions league. Milan pia itaanza msimu ujao ikiwa nyuma kwa point 15.