ROME: Karzai ameilamu Pakistan kuhusu Wataliban
17 Februari 2007Matangazo
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan kwa mara nyingine tena ameituhumu Pakistan kuwa haichukui hatua za kutosha kuwapiga vita wanamgambo wa Kitaliban katika maeneo ya mpakani.Akizungumza ziarani mjini Rome,Karzai amesema,mashambulio ya Wataliban yanayohofiwa kuwa yatashika kasi katika majira ya machipuko,hayawezi kufanywa bila ya msaada wa kigeni.Rais Karzai katika mazungumzo yake na viongozi wa serikali ya Italia,ameiomba serikali hiyo itoe msaada zaidi kwa Afghanistan. Hivi sasa,Italia ina wanajeshi 1,800 nchini Afghanistan.Ombi la NATO kuwa Italia iongeze idadi ya vikosi vyake Afghanistan,limekataliwa na Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi.