1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Marekani yatakiwa kuheshimu haki ya kujitawala ya Italia

2 Julai 2005

Italia imeiambia Marekani iheshimu haki ya kujiamulia mambo yake ya nchi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya majasusi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA kudaiwa kumteka nyara gaidi wa Kiislam mjini Milan hapo mwaka 2003.Waziri Mkuu wa Italia Slivio Berlusconi alimwita balozi wa Marekani aliyoko Italia Mel Sembler kwa mkutano wa karibu saa moja kufuatia madai kwamba Marekani ilivunja sheria ya Italia kwa kumnyakuwa sheikh mmoja wa Kiislam na kumpeleka nchini Misri ambapo waendesha mashtaka wanaamini aliteswa.Italia likanusha kujuwa na mapema juu ya kutekwa nyara kwa sheikh huyo.

Wiki iliopita hakimu wa Milan alitoa hati za kukamatwa kwa mashushu 13 wa CIA wanaotuhumiwa kutekeleza utekaji nyara huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW