ROME : Mashabiki wa soka wapambana na polisi
12 Novemba 2007Matangazo
Takriban mashabiki 200 wa soka nchini Italia wamezishambuli kambi za polisi mjini Rome.
Polisi imesema baadhi ya mashabiki hao waliokuwa wakivurumisha mawe na marungu wamewasha moto nje ya kambi zao na kuvunja madirisha ya majengo.Mashabiki hao pia walipambana na polisi nje ya uwanja wa soko jijini humo hapo jana.
Ghasia hizo zimezuka mara baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi na polisi shabiki mmoja wa timu ya Lazio wakati wa mapambano na mashabiki wa timu ya Juventus huko Tuscany.
Msemaji wa polisi amesema risasi aliyopigwa shabiki huyo ilifyatuka kwa bahati mbaya.
Kutokana na ghasia hizo mechi ya Lazio na Inter Milan imeahirishwa.