1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Mtuhumiwa wa ugaidi kurudishwa Uingereza

13 Septemba 2005

Mahkama ya Rufaa ya Italia imekubali ombi la Uingereza la kurudishwa nchini humo kwa mtuhumiwa wa uripuaji wa mabomu mjini London.

Hamdi Isaac atarudishwa nchini Uingereza katika kipindi kisichozidi siku 10 ambako anatakiwa kwa madai ya dhima aliyotimiza katika shambulio la Julai 21 katika mfumo wa reli wa mjini London.Isaac amekiri kushiriki katika uripuaji huo wa mabomu ulioshindwa mjini London lakini amesisitiza kwamba dhamira ilikuwa ni kuwatisha watu na sio kuwauwa.

Hakuna mtu aliyeuwawa katika mashambulizi ya mabomu hayo yaliyoshindwa kuripuka ambayo yalikuwa ni kuigiza mashambulizi ya tarahe 7 Julai ambapo watu zaidi ya 50 waliuwawa katika mji mkuu huo wa Uingereza.

Wakati huo huo habari kutoka Jakarta Indonesia zinasema kwamba mahkama nchini humo imemhukumu kifo mwanamgambo wa Kiislam kwa kula njama ya uripuaji wa bomu wa ubalozi wa Australia mjini Jakarta mwaka jana.

Iwan Darmawan Mutho amepatikana na hatia ya ugaidi na kuwaficha wahusika wa vitendo vya ugaidi.Mutho amekanusha kuhusika katika mripuko huo wa bomu lililotegwa kwenye gari ambalo limeuwa watu 10 na kujeruhi karibu 200.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW