1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME : Papa ajitokeza kwenye dirisha la hospitali

27 Februari 2005

Kwa mara ya kwanza kabisa Papa John Paul wa Pili tokea awe katika uongozi huo wa upapa miaka 26 iliopita hakuongoza sala za Jumapili za Bikira Maria na badala yake baraka za sala hiyo zimetolewa na msaidizi wake.

Askofu Mkuu Leonardo Sandri ametowa baraka hizo katika uwanja wa St.Peter na kusoma ujumbe wa maandishi kutoka kwa Papa aliyeko hospitalini ambao umewataka maelfu ya waumini waliokusanyika katika uwanja huo wa St.Peter kumuombea kwa kuwataka waendelee kuadamana naye na dua zao.

Wakati huo huo Papa amejitokeza kwa ghafla kwenye dirisha la hospitali ya Gemelii mjini Rome na kuwapungia umati wa watu waliokuwa nje kumuombea afya.

Papa John Paul wa Pili amekuwa hawezi kuzungunza tokea afanyiwe operesheni ya roho kwa ajili ya kumpa nafuu kwa matatizo yake ya kupumuwa.