ROME: Papa amesoma misa ya mkesha ya Pasaka
8 Aprili 2007Matangazo
Baba Mtakatifu Benedikt XVI amesoma misa ya mkesha ya Pasaka mjini Rome,ikihudhuriwa na maelfu ya waumini.Katika hotuba yake Papa alisema Ufufuo wa Yesu Kristo hudhihirisha kuwa upendo una nguvu zaidi kuliko maovu na kifo.Wakati wa misa hiyo ya mkesha,idadi kadhaa yaa watu walibatizwa na Baba Mtakatifu.Leo asubuhi Papa atatoa risala ya desturi ya Pasaka-“Urbi et Orbi”.