1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome. Papa Benedict arejea Rome.

15 Septemba 2006

Kiongozi wa kanisa Katoliki papa Benedict wa 16 amerejea mjini Rome baada ya kukamilisha ziara ya siku sita katika jimbo alikozaliwa la Bavaria kwa kufanya ziara katika kanisa kuu la mjini Munich katika kitongoji cha Freising, ambako alifanywa kuwa kasisi mwaka 1951.

Benedict amezusha mkanganyiko katika ziara hiyo wakati akitoa lawama kwa mbali kwa nadharia ya Kiislamu ya Jihad ama vita vitakatifu.

Lakini ziara hiyo itakumbukwa kuwa ni kurejea katika njia alikotokea katika kile kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 79 alipokiri kuwa huenda itakuwa ziara yake kuu ya mwisho katika eneo alikozaliwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW