ROME: Prodi amepewa nafasi mpya kuongoza serikali ya Italia
24 Februari 2007Matangazo
Rais Giorgio Napolitano wa Italia amemtaka Romano Prodi abakie kama waziri mkuu na aitishe kura mpya ya imani bungeni.Napolitano ametangaza uamuzi huo baada ya kukamilisha majadiliano ya dharura ya siku mbili pamoja na wanasiasa muhimu na kuhakikishiwa kuwa Prodi atakuwa na wingi wa kutosha bungeni.Siku ya Jumatano,Prodi alizusha mzozo wa kisiasa alipojiuzulu,baada ya kushindwa bungeni katika kura muhimu kuhusika na masuala ya sera za nje.Miongoni mwa masuala hayo ni kupelekwa kwa vikosi vya Italia nchini Afghanistan na kupanua kituo cha kijeshi cha Marekani nchini Italia.