Rome. Tony Blair akutana na Pope Benedict.
24 Juni 2007Matangazo
Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amekutana na kiongozi wa kanisa Katoliki Benedict wa 16 kwa faragha mjini Vatican. Taarifa ya makao makuu ya kiongozi huyo wa kidini mjini Vatican baadaye ilisema kuwa Benedict na Blair walijadili masuala kama mashariki ya kati, hali ya baadaye ya umoja wa Ulaya na sheria ambazo hazikutajwa zilizopitishwa hivi karibuni nchini Uingereza.
Mazungumzo hayo, ikiwa ni mara ya pili kukutana mwaka huu na Blair , yanakuja siku nne kabla ya kuondoka madarakani na yaligubikwa na fununu kuwa waziri mkuu huyo Muanglikani huenda akabadilisha madhehebu na kuwa Mkatoliki. Mke wa Blair Cherie ni muumini wa madhehebu ya Katoliki.