ROME : Utatanishi juu ya serikali ya Italia
19 Aprili 2005Kuna hali ya kutatanisha juu ya serikali ya Italia.
Hali hiyo inafuatia baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Silvio Berlusconi kushindwa kujiuzulu wakati wa mkutano wake na Rais Carlo Azeglio Ciampi.Berlusconi alikuwa akitarajiwa kujiuzulu na baadae kuchukua hatua ya kuunda serikali mpya.Lakini baada ya mkutano huo Rais Ciampi amesema Berlusconi anapaswa kurudi tena bungeni kuona kwa kiasi gani bado anaungwa mkono.
Repoti za awali zilidokeza kwamba Berlusconi amefikia makubaliano na mawaziri waasi wa chama cha Christian Demokrat UDC kujiunga na serikali mpya ya mrengo wa kulia wa wastani na hiyo kuepuka kuitisha uchaguzi mpya.
Mgogoro huo ulizidi kuwa mkubwa Ijumaa iliopita wakati mawaziri hao wa UDC walipojiuzulu.
Mawaziri hao wamekuwa wakidai kufanyika mabadiliko makubwa ya sera baada ya serikali yao ya mseto kushindwa vibaya katika uchaguzi wa mikoa wa hivi karibuni.