ROME: Wahamiaji wasio halali wazuiliwa nje ya Italia
5 Agosti 2007Matangazo
Maafisa nchini Italia wamesema,katika kipindi cha saa 24 wamewazuia zaidi ya watu 250,karibu na kisiwa cha Lampedusa,kusini mwa Sicily.Watu hao walijaribu kuingia Ulaya kwa njia zisizo halali. Boti tatu zilizokuwa na takriban watu 100 zilizuiliwa mapema siku ya Jumamosi.Na siku ya Ijumaa,boti zingine tatu zilikamatwa,zikiwa na watu 162 waliotaka pia kukimbilia Ulaya.Kisiwa cha Lampedusa,kusini mwa Italia,mara kwa mara hutumiwa kama mahala pa kuwashusha watu wanaotokea Afrika na kutaka kuanza maisha mapya barani Ulaya.