ROME: Wakimbizi wa Kikurd wakamatwa pwani ya Italia
25 Februari 2007Matangazo
Boti ya uvuvi iliopakia wakimbizi 130 wa Kikurd imewasili kusini mwa Italia.Polisi na wanajeshi wa Italia waliwakamata wakimbizi hao kwenye pwani ya Calabria,wengi wao wakiwa ni wanaume.Wamesema kuwa safari ya boti hiyo ilianzia Uturuki,juma moja lililopita.