ROME : Wamorocco watatu mbaroni kwa ugaidi
22 Julai 2007Matangazo
Polisi ya Italia imewakamata wanaume watatu wanaotuhumiwa kuendeshchuo chuo cha ugaidi katika mji wa Perugia na wanamsaka mtuhumiwa wa nne.
Watu hao watatu ambao wote ni Wamorocco wanatuhumiwa kuendesha chuo hicho katika msikiti pamoja na imamu.Polisi inasema wamegunduwa ushahidi wa mafunzo ya kina juu ya mabomu na sumu na maelekezo ya kurusha ndege aina Boeing 747.
Mtu wa nne hivi sasa inaaminika kuwa yuko katika nchi nyengine.