ROME : Watetezi wa familia nusu milioni waandamana
13 Mei 2007Matangazo
Maelfu ya wananchi wa Italia wameandamana mjini Rome kupinga muswada wa sheria ambao utatowa haki zaidi kwa watu wanaoishi pamoja bila ya kufunga ndoa wakiwemo mashoga.
Muswada huo ambao ni kitovu cha utata uliidhinishwa na serikali ya sera za wastani za mrengo wa shoto ya Waziri Mkuu Romano Prodi hapo mwezi wa Februari.Unajumuisha haki za ziara za hospitali na urithi.
Makundi ya Kikatoliki na yale ya kifamilia yameandaa maandamano hayo hapo jana ambayo yamehudhuriwa na wana siasa mashuhuri wa kihafidhina akiwemo mtagulizi wa Prodi Silvio Berlusconi.