Rome. Waziri mkuu wa Italia atakiwa kuja na mpango mpya katika serikali yake.
17 Aprili 2005Matangazo
Nchini Itali, chama cha Christian Democrats , UDC kimedai kuwa waziri mkuu Silvio Berlusconi aunde serikali mpya na kuleta mipango mipya. Wito huo unakuja baada ya mawaziri wanne wa chama hicho, ikiwa ni pamoja na naibu waziri mkuu Marco Follini, kujiondoa katika muungano wa serikali inayoongozwa na waziri mkuu Berlusconi. Hili ni pigo la hivi karibuni kabisa dhidi ya Bwana Berlusconi kufuatia kushindwa vibaya katika uchaguzi wa majimbo wiki iliyopita. Berlusconi alichaguliwa mwaka 2001 akiongoza serikali inayoundwa na vyama vinne, akiahidi kuleta mageuzi na kubadilisha uchumi wa Italia unaoyumbayumba.