ROME.Berlusconi aonekana kuyumba na msimamo wake wa kuondoa wanajeshi wa Italia kutoka Iraq
17 Machi 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa Italia,Silvio Berlusconi ameonekana kuyumba na msimamo wake juu ya pendekezo lake la kuviondoa vikosi vya jeshi la Italia kutoka Iraq.Berlusconi alisema siku ya Jumanne wiki hii kuwa nchi yake itaanza kuviondoa vikosi vyake kutoka Iraq kuanzia mwezi wa Septemba mwaka huu.Lakini baadae akasema bado haijawekwa tarehe maalum ya kuviondo vikosi hivyo na kuwa suala lolote linalohusu uondoaji wa vikosi vya Italia ni lazima kwanza likubaliwe na nchi nyingine washirika wa Marekani huko Iraq.