ROME:Homa ya ndege barani Afrika?
27 Oktoba 2005Matangazo
Watalaamu wametabiri kwamba bara la Afrika litakumbwa na vijidudu vya ugonjwa wa homa ya ndege baada ya bara la Asia.
Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema ugonjwa huo unaweza kuingizwa katika Mashariki ya Kati na Afrika Mashariki mnamo muda wa wiki chache.
Wataalamu wametahadharisha kwamba madhara ya ugonjwa huo kiafya na kiuchumi huenda yakawa makubwa zaidi barani Afrika kuliko katika nchi za Asia.
Sehemu ambazo hasa zinaweza kuathirika ni za mkoa wa Rift Valley katika Africa Mashariki zinazotegemea sana ufugaji wa kuku ili kuendesha maisha.
.