ROME:Mazungumzo juu ya mpango wa Nuklia wa Iran yafanyika Roma
23 Oktoba 2007Matangazo
Mkuu wa sera za nje katika Umoja wa Ulaya Javier Solana anakutana leo hii na mpatanishi mkuu wa Iran kwenye mazungumzo ya Nuklia ya nchi hiyo mjini Roma Italia.
Mpatanishi huyo Saeed Jalili anatazamiwa kuwa na msimamo mkali kutokana na kuwa mtu wa karibu wa rais wa Iran Mahmoud AhmadNejad.Kabla ya kikao cha leo mjumbe huyo wa Iran amenukuliwa akisema kwamba hatazungumza na yeyote juu ya haki ya Iran kuwa na technologia ya Nuklia.Wakati huo huo waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amefanya mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Israel Ehud Olmert mjini London na zaidi walichokizungumzia ni suala la Nuklia ya Iran.