Ronaldo afikishwa mahakamani
31 Julai 2017Ronaldo ndiye mchezaji wa karibuni kujikuta taabani na mtoza kodi wa Uhispania. Nyota huyo Mreno mwenye umri wa miaka 32 aliulizwa maswali na mahakama ya Pozuelo de Alarcon, kitongoji cha kitajiri cha mji wa Madrid, ambako anaishi, baada ya kurejea kutoka mapumzuko wa kipindi cha joto. Ronaldo amemwambia jaji kuwa hajawahi kujaribu kukwepa kodi. ÑAKI TORRES ni msemaji wa nyota huyo,
Nna maneno machache tu ya kusema, mchezaji huyo ametoa ushahidi wake. Kila kitu kiko shwari na tayari yuko njiani kwenda nyumbani na katika dakika chache zijazo tutatoa kwa vyombo vya habari taarifa ikatayokuwa na maelezo kamili.
Ronaldo, -- mwanamichezo anayelipwa kitita kikubwa kabisa cha pesa duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes – anafuata katika nyayo za hasimu wake mshambuliaji wa Barcelona Muargentina Lionel Messi, ambaye alikutikana na hatia ya kosa kama hilo mwaka jana.
Waendesha mashitaka wanamtuhumu Ronaldo kwa kukwepa kulipa kodi ya dola milioni 17.3. Wanadai aliitumia fursa ya mfumo wa kampuni ulioundwa mwaka wa 2010 kuyaficha mapato yake anayoingiza Uhispania kutokana na haki zake za matangazo ya kibiashara.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri:Yusuf Saumu