1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rosberg asaini mkataba mpya na Mercedes

18 Julai 2014

Dereva wa mashindano ya mbio za magari ya Formula One, Mjerumani Nico Rosberg, hajawahi kushinda katika ardhi ya nyumbani na wikendi hii amejiandaa vilivyo kushiriki katika mkondo wa Hockenheim.

Formel Eins Qualifying in Silverstone Rosberg
Picha: REUTERS

Anashindana na dereva mwenzake wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton katika kinyang'anyiro cha kuwania taji la dereva bora ulimwenguni.

Mjerumani Nico Rosberg amesaini mkataba mpya wa “miaka kadhaa” na timu ya Mercedes. Rosberg anaongoza msururu wa ubingwa wa madereva akiwa na points nne kabla ya mashindano ya mkondo wa German Grand Prix.

Dereva huyo mwenye umri wa miaka 29, anayetafuta taji lake la kwanza la ubingwa wa ulimwengu, ameshinda mikondo mitatu ya msimu huu. Huenda akawa dereva wa kwanza kushinda katika mkondo wa nyumbani akiwa katika gari lililotengenezwa Ujerumani tangu mwaka wa 1939.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef