1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al-Sisi alithibitisha kugagombea muhula wa tatu Misri

3 Oktoba 2023

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi alithibitisha kugagombea muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Disemba.

Ägypten | Anhänger Präsident Abdel Fattah al-Sisi
Picha: Sayed Hassan/dpa/picture alliance

Sisi, mkuu wa zamani wa jeshi ambaye amekuwa rais tangu 2014, alikuwa anatarajiwa sana kugombea tena kwa muhula wa tatu baada ya marekebisho ya katiba ya miaka minne iliyopita ambayo ingeruhusu asalie madarakani hadi 2030.Katika majuma ya  hivi karibuni, wafuasi wake walianzisha kampeni kwa kutumia mabango na jumbe za umma zikimsihi Sisi awanie katika uchaguzi huo ujao.Sisi aliingia madarakani baada ya kuongoza juhudi za kutimuliwa kwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Mursi wa chama cha udugu wa Kiislamu mwaka 2013.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW