RSF: Ghasia dhidi ya waandishi Kongo zinaongezeka
26 Machi 2026
RSF imesema waandishi wote wa mashariki mwa Kongo iliowahoji, wameripoti kwamba tangu kukamatwa kwa Goma mnamo Januari 2025, mbinu zao za kufanya kazi zimebadilika kabisa.
Imeongeza kuwa takriban waandishi wanane wamezuiwa na kundi la waasi la M23 ama huduma za kijasusi za jeshi la kawaida kwa siku kadhaa.
Kulingana na ripoti iliyochapishwa siku ya Jumanne, RSF imesema waandishi wawili walifungiwa na M23 kwenye makonteina yaliogeuzwa kuwa jela ambapo hadi wafungwa 80 walifungiwa kwa pamoja.
Ripoti hiyo pia imesema M23 iliwapa takriban waandishi wanne mafunzo ya kiitikadi, kudhibiti vipindi kwenye vituo vya redio vya ndani, na kulazimishia vipindi fulani au hoja za kuzungumzia
Wakati huo huo, ripoti hiyo imesema serikali imewashtumu waandishi wa habari kwa kuegemea upande wa M23 na washirika wake wa Rwanda.