1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RSF: Idadi ya juu zaidi ya wanahabari walikamatwa mwaka 2021

16 Desemba 2021

Jumla ya waandishi wa habari 488 wamekamatwa na kufungwa mwaka huu kutokana na taaluma yao.

Belarus | Journalisten halten eine Ausgabe des Komsomolskaya Pravda
Picha: Natalia Fedosenko/TASS/dpa/picture alliance

Hayo ni kulingana na ripoti ambayo imetolewa na shirika la waandishi wa habari wasiokuwa na mipaka RSF. RSF imetoa tahadhari kwamba China, Belarus na Myanmar ni miongoni mwa nchi zenye sifa mbaya zaidi za kuwafunga jela waandishi wa habari.  

Hali si shwari kwa waandishi wa habari. Tawala kandamizi kama za Belarus, China na Myanmar zinatumia nguvu kukandamiza juhudi za kidemokrasia katika nchi zao, huku uhuru wa kujieleza ukibanwa.

Katika mataifa ya magharibi mathalan Marekani na vilevile Ulaya wanaoeneza siasa za kizalendo wanaendelea kutishia uhuru wa habari hasa katika kipindi hiki cha janga la COVID-19.

Shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka (RSF) limetoa tahadhari katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu machafuko na ukiukwaji wa haki dhidi ya wanahabari.

Mauaji ya wanahabari yapungua

Ripoti ya RSF kuhusu uhuru wa vyombo vya habari imesema zaidi ya wakati wowote ule, waandishi wa habari kwa sasa wanakamatwa kiholela wanapofanya kazi zao.

Katika mwaka huu wa 2021, jumla ya waandishi habari 41 wameuawa. Hii ni idadi ya chini zaidi ya mauaji dhidi ya waandishi wa habari katika miaka mingi. Sababu moja iliyochangia hali hiyo kulingana na RSF ni kutokana na kupungua kwa migogoro ya kikanda mfano nchini Syria, Iraq na Yemen.

Katja Gloger ambaye ni mwanachama wa bodi ya RSF ameongeza kuwa nchi ambazo ni hatari zaidi ni kama Mexico ambako wanahabari saba waliuawa na Afghanistan ambako wanahabari sita waliuawa. Yemen na India, zikirekodi mauaji ya waandishi habari wanne kila moja mwaka 2021.

Takriban waandishi Habari 65 wanaaminika kutekwa nyara, hasa nchini Syria, Iraq na Yemen.

Idadi kubwa ya waandishi Habari wawekwa kizuizini

Jumla ya waandishi Habari 488 wamekamatwa na kuwekwa kizuizini ulimwenguni kote kuhusiana na taaluma yao katika mwaka 2021.

Jumla ya waandishi Habari 488 wamekamatwa na kuwekwa kizuizini ulimwenguni kote kuhusiana na taaluma yao. Hii ndiyo idadi ya juu zaidi ambayo RSF imewahi kurekodi ya waandishi Habari waliofungwa. Ripoti inafafanua kwamba 103 si waandishi wa Habari kitaaluma bali ni wanaharakati ambao hutoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha kulingana na ripoti hiyo, idadi ya waandishi habari wa kike waliofungwa jela pia imeongezeka kwa theluthi moja.

Watuhumiwa wakuu: China, Belarus na Myanmar

Shirika la RSF limetaja mataifa matano ambayo visa vya ukamataji wa waandishi Habari viliongezeka. Ikiwa ni Pamoja na China ambapo jumla ya wanahabari 127 waliwekwa kizuizini, Myanmar iliwafunga wanahabari 53, Belarus ikawafunga 32, na vilevile Vietnam na Saudi Arabia zipo kwenye orodha hiyo.

Ripoti imeeleza kwamba ongezeko hilo la wanahabari wanaofungwa kiholela latokana na misimamo ya serikali za nchi hizo kutofautiana na matakwa ya demokrasia miongoni mwa wananchi.Picha: AP Photo/picture alliance

Isitoshe ukubwa wa idadi hiyo ya ukamataji inaashiria pia ongezeko la ukandamizaji dhidi ya vyombo huru vya habari.

Katika kisa cha hivi karibuni kilichogonga vichwa vya Habari, mahakama ya Belarus ilimhukumu mwanablogu maarufu Siarhei Tsikhanouski kifungo cha miaka 18 jela.

Nchini Myanmar, idadi ya waandishi Habari ambao wamefungwa imeongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi.

Visa nchini China vimechochewa Zaidi na hatua ya Rais Xi Jinping kuendeleza udhibiti wake wa Hong Kong.

(RSF)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW