1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RSF imefanya mauaji ya kimbari - Marekani

8 Januari 2025

Marekani imesema kuwa ina ushahidi wa kutosha kwamba wapiganaji wa Kikosi cha Dharura nchini Sudan, RSF, wamefanya mauaji ya kimbari na imetangaza vikwazo dhidi ya kiongozi wa kundi hilo.

Sudan | Mohamed Hamdan Daglo
Kiongozi wa RSF, Mohamed Hamdan Daglo.Picha: Ashraf Shazly/AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, amesema uamuzi huo unatokana na ushahidi wa mauaji ya wanaume na wavulana yanayofanywa na RSFna ubakaji wa wanawake na wasichana wa makabila maalum nchini Sudan.

Blinken amesema kwenye taarifa yake ya jana kwamba Marekani inamuwekea vikwazo kiongozi wa RSF, Muhammad Hamdan Daglo, maarufu kama Hemedti, kwa jukumu lake kwenye mateso dhidi ya watu wa Sudan.

Soma zaidi: RSF yasema imechukua udhibiti kwa mara nyingine eneo la kaskazini mwa Darfur

Kwa mujibu wa vikwazo hivyo, Hemedti na familia yake wamezuiwa kuingia Marekani.

Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kinga na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari uliotiwa saini baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, unayatafsiri mauaji ya kimbari kama matendo yanayotendwa kwa lengo la kuharibu, kikamilifu au kwa sehemu, kundi la kitaifa, kikabila au kidini. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW