1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhuru wa vyombo vya habari

RSF: Waandishi wa habari 67 waliuawa miezi 12 iliyopita

9 Desemba 2025

Waandishi wa habari sitini na saba wamepoteza maisha kutokana na kazi zao katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, wengi wao wakiwa ni wahanga wa vita au mitandao ya uhalifu.

Tunisia Tunis 2025 | Picha za waandishi wa habari wa Al Jazeera waliopigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano dhidi ya Israel katika msafara wa Flotilla ya Global Sumud
Picha za waandishi wa habari wa Kipalestina wa Aljazeera waliouawa zinaonyeshwa katika mkutano wa kulaani kitendo cha Israel kuuzuia msafara wa misaada ya kiutu wa Global Sumud Flotilla (GSF), uliokuwa ukielekea Ukanda wa GazaPicha: Fethi Belaid/AFP/Getty Images

Kulingana na Shirika la haki za waandishi wa habari wasio na mipaka (RSF) leo Jumanne, takwimu hizi za kati ya mwanzo wa Disemba 2024 hadi mwanzo wa Disemba mwaka huu zinalinganishwa na kipindi cha miezi 12 iliyotangulia.

Eneo ambalo lilikuwa hatari zaidi kwa waandishi linasalia kuwa ni Ukanda wa Gaza ambako waandishi 29 waliuawa, ikifuatiwa na Mexico iliyokuwa na vifo 9.

Mkuu wa RSF nchini Ujerumani Anja Asterhaus amezitolea wito serikali kote ulimwenguni kuchukua hatua na kuongeza kuwa ikiwa wale wanaotoa ripoti za ukosoaji wanahofia uhuru wao ama maisha yao, ni dhahiri demokrasia iko mashakani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW